Dk Mlay, amesema katika tukio hilo hospitail hiyo imepokea majeruhi 10, kati yao 9 ni wanaume na mwanamke mmoja aitwaye Sharifa Jumanne, ambaye hali yake imeelezwa kuwa mbaya. Amesema kuwa katika uchunguzi wa awali imegundulika kuna kuipande cha chuma kwenye mapafu ambacho kinatokana na mlipupuko huo.
Aidha, amesema kuwa majeruhi mwingine aliyepata majeraha ya kichwa amehamishiwa kwenye hospitali ya Seliani ya Arusha kwa uchunguzi zaidi akisubiriwa kupelekwa kwenye hospitali ya rufani ya KCMC, Moshi.
Dk Mlay, amesema hali za majeruhi wengine waliolazwa katika hospitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru, zinaendelea vizuri.
Mkuu wa Mkoa, Magesa Mulongo, amewatembelea majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa mahospitalini.
Viongozi mbalimbali wa CHADEMA wametembelea eneo la tukio.
SOURCE: CHADEMA SOCIAL MEDIA
No comments:
Post a Comment