Wafanya kazi za uokozi wanatoboa shimo kwenye kifusi kujaribu kuwafikia haraka manusura walionasa wakati jengo hilo lilipoanguka.
Baadhi ya waokozi wameondolewa kwa sababu hawakuweza kuhimili uvundo mkali wa maiti zilizooza ndani ya kifusi.
Watu 2400 wamenusuriwa tangu jengo hilo la ghorofa nane kuporomoka mjini Dhaka.
Zaidi ya watu 360 wanajulikana kuwa wamekufa.
Msemaji wa jeshi la Bangladesh, Brigadier General Siddiqul Alam Sikder, alisema hawataondoa kifusi kwa sasa, ila katika kusaidia kumuokoa mtu:
"Hatutaondoa chochote hadi tuna hakika kwamba hakuna mtu aliye bado hai ndani ya kifusi.
Makundi yote yanayofanya uokozi chini ya kifusi yatatuarifu.
Tukipata taarifa hiyo, tutakutana kuamua kama tutaingia kwenye kifusi, au tunyanyue paa kwa crane.
Kisha tutaingia kipindi cha pili cha operesheni."
SOURCE: BBC Swahili
No comments:
Post a Comment