Mkutano mkuu wa UEFA unaoshirikisha nchi wanachama 53 umepangwa kufanyika huko jijini London siku ya ijumaa ya tarehe 24/05/2013 na agenda za mkutano huo zimekwisha tolewa. Mkutano huu wa 37 unategemewa kufanyika katika hoteli ya Grosvenor House, Park Lane huko London.
Nchi 53 wanachama wa UEFA hukutana kila mwaka, na kwa mwaka huu ajenda zitakazojadiliwa ni pamoja na:
- Ripoti ya mwaka ya rais wa UEFA na kamati kuu na ripoti ya kiutawala ya UEFA kwa mwaka 2011/2012
- Ripori ya kazi za kamati za UEFA
- Maswala ya fedha yakihusisha bajeti kwa mwaka 2013/2014
- Uchaguzi wa kamati kuu
- Swala la ubaguzi wa rangi kwa soka la ulaya
- Maombi ya uanachama wa chama cha mpira wa miguu cha Gibraltar kwa UEFA
kamati kuu ya UEFA inategemewa kukutana tarehe 22 na 23 mwezi huo wa tano kabla ya mkutano mkuu.
SOURCE: UEFA website
No comments:
Post a Comment