| Sirefina Diediou alijiunga na kikosi cha taifa mwaka jana. Anasema likuwa anapigana na vijana alipokuwa shuleni na ilimchukua mamake muda kukubali kuwa anapenda mchezo huu. |
| Wasichana wadogo pia walishiriki miereka kujifurahisha tu kwa sababu kulikuwa na zawadi kama baiskeli, saa na komputa za kushindaniwa |
| Kuvutana nywele hairuhusiwi wakati wa miereka lakini refarii haonekani kama anawatizama wawili hawa. |
| Wasichana wanapaswa kuvua mikufu yao lakini baadhi yao wanapuuza sheria |
| Wasichana wengi huwa hawashiriki miereka kwa sababu ya kwenda shule au katika vyuo vikuu na wengine kwa sababu ya mimba za mapema |
| Mengi ya mavazi wanayovalia wanaume huwa ina maana yake, wanaume hawa hata hivyo wamevalia mavazi haya ili kuwaletea bahati njema waweze kushinda |
| Densi hii inapaswa kuonyesha wanaume walivyo wakakamavu tayari kwa miereka |
| Zamani mchezo huu haukuwa na refari kwani mashabiki ndio wangeamua mshindi lakini siku hizi mambo yamebadilika kwani marefa ndio wanaamua mshindi |

