GARETH BALE |
Mshambuliaji matata wa Tottenham Hotspur Gareth Bale ametajwa kuwa mchezaji bora wa mwaka na chama cha waandishi wa habari za michezo nchini England.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, kutoka Wales, ameshidna tuzo hiyo wiki moja tu baada ya kushinda mataji ya mchezaji bora wa mwaka wa shirikisho la mchezo wa soka nchini England FA, na pia taji mwa mchezaji bora mchanga mwaka huu.
Bale amefunga magoli 19, baada ya kucheza mechi 29, za ligi kuu ya Premier msimu huu.
Mshambulizi wa Manchester United Robin van Persie, ambaye alishidna tuzo hilo mwaka uliopita alimaliza katika nafasi ya pili naye Juan Mata wa Chelsea akiwa wa tatu.
Bale ameisaidia klabu yake ya Tottenham kufika robo fainali ya kuwania kombe la Uropa na pia kusalia miongoni mwa timu nne bora kwenye msururu wa ligi kuu ya Premier.
Kocha wa Tottenham Andre-Villas-Boas, anaamini kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Southampton atasalia katika klabu hiyo hata ikiwa hawatamaliza katika nafasi nne bora na kukosa nafasi ya kushiriki katika fainali za kuwania kombe la klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao.
SOURCE: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment