Bw.Henry Kileo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza. |
Ulinzi katika Mahakama hiyo uliimarishwa ipasavyo. |
Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na watuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013 |
Na Josephat Isango wa Tanzania Daima.
KAIMU
Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa Dar es
Salaam, Henry Kilewo, anashikiliwa na polisi , akihusishwa na tukio la
kumwagiwa tindikali, Musa Tesha. Tesha alimwagiwa tindikali na watu
wasiojulikana Septemba 9, mwaka juzi kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo wa
Jimbo la Igunga, uliomuweka madarakani Dk. Kafumu Dalali.
Akizungumza
juzi na Tanzania Daima kabla ya kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi,
Kilewo alisema hajui anachoitiwa na kwamba anatekeleza wito wa jeshi
hilo kuwa afike ofisini kwao. “Sijui ninachoitiwa, nimepigiwa simu
naenda kutekeleza wito, nimesha wataarifu mawakili wangu ninaowaamini,
kwa kuwa chochote kinaweza kutokea cha msingi Watanzania wapenda mageuzi
waniombee kwa Mungu,” alisema Kilewo.
Wakili
wa Kilewo, Peter Kibatala, alisema baada ya mteja wake kuhojiwa kwa
muda wa saa tano juzi alielezwa kuwa anapelekwa Igunga, mkoani Tabora
kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi ya kutumia tindikali na
kujeruhi.
Kibatala
alisema anasikitishwa na hatua ya jeshi hilo kumnyima dhamana mteja
wake ilhali kosa wanalomtuhumu linadhaminika na kwamba hayo ni matumizi
mabaya ya madaraka kumzuia mtu kwa zaidi ya saa 24 pasipo kumfikisha
mahakamani. Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za
kutumia tindikali na kudhuru watu ni pamoja na Oscar Kaijage wa
Shinyanga na Evodius Justinian wa Bukoba.
No comments:
Post a Comment