Mabingwa wa Afrika, timu ya taifa ya Nigeria imeondolewa kwenye michuano ya kombe la mabara baada ya kutandikwa mabao 3-0 na mabingwa wa dunia Hispania.
Mabao mawili ya beki wa klabu ya Barcelona,
Jordi Alba na moja la mshambuliaji wa Chelsea, Fernando Torres yalitosha
kuzamisha jahazi la Nigeria ambao wameshinda mechi moja pekee dhidi ya
Tahiti wikiendi iliyopita.
Nigeria wameyaaga mashindano hayo
baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye kundi B wakiwa na pointi
tatu nyuma ya Uruguay walioko kwenye nafasi ya pili wakiwa na point
sita.
Hispania ni vinara wa kundi B wakiwa wamemaliza
hatua ya makundi na ushindi wa asilimia mia moja wakiwa na pointi tisa
ambapo sasa watakwenda kuwavaa Italia katika hatua ya nusu fainali ya
michuano hiyo hapo siku ya siku ya alhamisi mjini Fortaleza.
Uruguay wao wametoa kipigo cha magoli 8-0 kwa
timu wachovu kwenye michuano hiyo Tahiti ambao wameondoka na jumla ya
magoli 24 ya kufungwa na kupata bao moja pekee walipocheza na Nigeria.
Kwa matokeo hayo, Uruguay watacheza nusu fainali dhidi ya wenyeji Brazil, hapo siku ya jumatano.



No comments:
Post a Comment