Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon amelaani
vikali mashambulizi dhidi ya ofisi za umoja wa mataiofa mjini Mogadishu
Somalia.
Ban amesema kupitia kwa msemaji wake kuwa
shambulizi hilo lilikuwa kitendo cha unyama, na ambacho kilisababisha
vifo vya watu 15.
Kwa Mujibu wa msemaji wake Ban,pia
alisisitiza kuwa Umoja wa mataifa hautaogopa kutokana na mashambulizi
hayo kuendelea na kazi zake nchini Somalia.
Washambuliaji walishambulia ofisi hizo kwa
kulipua gari lililokuwa limeegeshwa karibu na lango kuu la ofisi zenyewe
na kisha kuanza kukabiliana na maafisa wa usalama kwa kufyatuliana
risasi ndani ya ofisi hizo.
Kwingineko mjumbe maalum wa Mwenyekiti wa Tume
ya Umoja wa Afrika (SRCC) nchini Somalia, Balozi Mahamat Saleh Annadif
ameshutumu vikali shambulio la kigaidi lililofanywa leo na magaidi wa
Al-Shabaab katika makao ya Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu.
"Tunalaani vikali shambulio hili la kinyama
katika makao ya Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu. Mashambulio haya
yasiyofanikiwa yanayoendeshwa na Al-Shabaab yanalenga tu kuvuruga
jitihada zinazochukuliwa na wananchi wa Somalia baada ya vita vya
wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya ishirini na magaidi hao
hawawezi kuzuia jitihada zetu za pamoja kuendelea kuwasaidia wananchi wa
Somalia kuijenga nchi yao" amesema Mwakilishi Maalum wa Mwenyekiti wa
Umoja wa Afrika nchini Somalia (SRCC), Balozi Mahamat Saleh Annadif.
Balozi Mahamet Annadif amepongeza hatua ya
haraka iliyochukuliwa na majeshi maalum ya AMISOM na majeshi ya usalama
ya Somalia na amesisitiza kuwa AMISOM haitaacha kuchukua hatua za
kuimarisha usalama nchini Somalia.
"Umoja wa Afrika na AMISOM kwa sasa wako pamoja
na wananchi wa Somalia," amesema Balozi Annadif, wakati akituma salaam
za rambirambi kwa wale waliowapoteza wapendwa wao katika shambulio hilo
na kuwaombea kupona haraka watu wote waliojeruhiwa.
Takriban watu 12 wakiwemo ria wa kigeni wameuawa
katika shambulizi baya lililofanywa dhidi ya ofisi ya umoja wa mataifa
mjini Mogadishu Somalia
Ufyatulianaji risasi uliodumu kwa zaidi ya saa
moja ulishuhudiwa ndani ya ofisi za shirika la maendeleo la umoja wa
mataifa UNDP.
Mpiga picha aliyeshuhudia kisa hicho, aliambia
BBC kuwa mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua ndani ya gari moja
liliokuwa karibu na lango kuu la ofisi hizo na kuwa aliona washambuliaji
wanne wakiingia ndani ya ofisi yenyewe.
Kundi la Al Shabaab limesema kuwa ndilo lilifanya shambulizi hilo.
Somalia haijakuwa na serikali thabiti kwa zaidi ya miaka 20, na kipindi hicho chote nchi hiyo ilikuwa eneo la vita.
Lakini sasa serikali inapata msaada kutoka kwa
umoja wa mataifa na imeweza kudhibiti miji mingi ya nchi hiyo na hata
kufurusha wapiganaji wa al-Shabaab.
Hata hivyo waziri mkuu Abdi Farah Shirdon Saaid,
amesema kuwa Al Shabaab haiwezi kushinda vita dhidi ya serikali
inayojaribu kuleta utulivu na amani nchini kote
Ofisi kuu ya shirika la UNDP, iko karibu na eneo lenye ulinzi mkali karibu na uwanja wa ndege Kusini mwa Mogadishu.
Baadhi ya wale waliouawa na wafanyakazi wa UN, majengo pia yameharibiwa na watu wamelazimika kukimbilia usalama wao.
SOURCE: BBC
SOURCE: BBC
No comments:
Post a Comment